WIKI iliyopita tulieleza majini ni viumbe gani na wanaishi sehemu gani hapa duniani.
Njia mojawapo ni kama kwa Remote Control; Hii inamfanya yule aliyedhibitiwa na majini kuweza kuelewa au kuwa na fahamu zake lakini anakuwa hawezi kuudhibiti mwili wake na huwa anasema yale anayotaka yule jini.
Njia ya pili ni jini humuingia binadamu kupitia kwenye utosi na kuingia katika mfumo wa damu. Linapoingia kwa njia hii binadamu hupoteza fahamu na kuwa zezeta na anakuwa haelewi kabisa kinachoendelea. Anachokifanya ni kile anachotaka jini.
Kuna njia nyingine ambayo jini hukaa nyuma ya binadamu na mtu huyo huwa hapotezi fahamu ila anakuwa hawezi kufanya lolote na mwili wake.
Majini vilevile wana uwezo wa kusafiri kwa kasi ya upepo bila kutumia chombo chochote; Binadamu hana uwezo huo isipokuwa kwa msaada wa majini.
Kwa kifupi ni kwamba yote yanayofanywa na wachawi na wanga humu duniani hayawezekani isipokuwa kwa msaada wa majini.
Jambo la muhimu ni kwamba pamoja na uwezo mkubwa walionao majini, wanadamu wana uwezo wa kuyatawala na kuyadhibiti kwa kutumia utaalamu maalum.
SOMA ZAIDI KUPITIA GLOBAL PUBLISHER.
0 comments:
Post a Comment