Stori:Mwandishi Wetu,MbeyaLORI aina ya Scania limeingia chumbani katika nyumba moja kijijini Ilonga, wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya na kuua watu watatu wa familia moja waliokuwa ndani.
Tukio hilo lilitokea Jumatatu iliyopita saa tatu na robo usiku ambapo
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki
amethibitisha na kuwataja marehemu kuwa ni Asia Yahya (52), wanafunzi wa
Shule ya Msingi Ilonga, Abubakari Yahaya (8) na Fatuma Yahaya (6).(PICHA NA MBEYA YETU)


0 comments:
Post a Comment