KWA nini majina yaleyale katika mistari hii? Ni kutokana na kile kinachojiri. Kuna baadhi ya mastaa Bongo ni vigumu kukwepa kuwazungumzia kutokana na drama zao za kila kukicha. Unaweza ukakwepa kuwazungumzia Wema Sepetu, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Khaleed Mohamed ‘TID’ gazetini lakini wakawa wametawala kwenye mitandao ya kijamii. Kwa nini? Ni kwa sababu hawakosi vitimbi. Kama siyo kufumwa wakifanya vitu vya ajabu, basi watakuwa wanagombana.
NESHIIII!!!!
MWIGIZAJI mwenye mvuto, Yobunesh Yusuf ‘Neshi’ amesema anatamani sana
kufanya kazi na Mbongo Fleva, Ambwene Yesaya ‘AY’ kwani anamvutia.
Akizungumza na Stori 3, Neshi alibainisha kuwa licha ya AY kufanya
muziki na yeye filamu, muonekano wa staa huyo umekuwa ukimvutia kuigiza
naye muvi.
“Yaani siyo siri AY ananivutia sana, ipo siku nadhani
nikifanikiwa kuzungumza naye na akakubali basi nitafanya naye kazi,”
alisema Neshi.
0 comments:
Post a Comment