Ripoti ya mtangazaji wa Radio One na ITV Reuben Mchome kupitia mchomeblog.com
imeamplfy kwamba ajali hii ilitokea Mto Wami baada ya tela la lori hili
la mafuta kukatika na kuponea kwa asilimia ndogo sana kuzama kwenye mto
huo ambao kwenye ripoti kadhaa umeripotiwa kuwa na Mamba.
Mpaka
lori hilo linaondolewa kwenye eneo la ajali, maelfu ya abiria walikwama
kwa muda wa zaidi ya saa sita ambapo kwa pande zote mbili watu
walilazimika kusubiri na foleni ilikua kubwa sana pia.
Mwaka
jana kulikua na taarifa ya lori la mkaa kugonga kuta za mto huo na
kuzama huku likiwa na kondakta wake pamoja na dereva waliodaiwa
kufariki.
0 comments:
Post a Comment