SIKU chache baada ya kuripotiwa akijiachia kimalavidavi na ‘lejendari’
wa Bongo Fleva, Aboubakar Katwila, staa wa muziki na filamu za Kibongo,
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amenaswa hotelini na bwana Mzungu aliyetajwa
kwa jina moja la George, kamera za Risasi Mchanganyiko ni noma.
Kwa
mujibu wa shushushu wetu, tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika
hoteli moja maarufu jijini hapa ambapo Shilole alikuwa kwenye ziara ya
shoo yake.
Ilidaiwa kuwa mara tu baada ya kumaliza ziara ya shoo,
Shilole hakuondoka jijini hapa na badala yake alionekana sehemu tofauti
akijivinjari na jamaa huyo ambaye uchunguzi wetu ulibaini kuwa ni bosi
wa klabu moja maarufu ya usiku Kanda ya Ziwa.
Kabla ya kuondoka
katika jiji hili la sangara na sato, Alhamisi iliyopita na ndege ya
jioni, Shilole alinaswa kimalavidavi na Mtasha huyo Jumatano katika
Ukumbi wa Mwalimu Nyerere wa Gold Crest kulipokuwa na maonesho ya
Biashara ya Kimataifa ya Syria.
Shilole alishuhudiwa akifanyiwa
‘shopping’ ya kufuru na bwana huyo ambapo gazeti hili lilinasa mpango
mzima ambapo lilipotaka kujua kama ni wapenzi, Mtasha huyo alijibu kwa
kifupi sana: “No comment” (sina la kusema).
Kwa upande wake Shilole
alipobanwa mbavu alifunguka: “Nisingependa kuongelea jambo hilo kwani
sasa najipanga kimuziki zaidi, shopping ni mambo ya kawaida sana kwa
hiyo ni vyema tukaongelea muziki wangu kwani shoo yangu ya Pasaka ilijaa
mashabiki wa kufa mtu so nakubalika sana Mwanza na siku moja nitaweka
makazi hapa.”
0 comments:
Post a Comment