WAZEE WANAOSADIIWA KUWA NI WACHAWI WAKIWA CHINI YA ULINZI KITUO CHA
POLISI,KUTOKA KUSHOTO NI MWAJUMA MPONI (70) NA KULIA NI SHIJA NKWABI
(80)
|
Watu wawili wamenusurika
kuuwawa usiku wa kuamkia juzi katika kijiji cha Mhongolo wilaya ya kahama mkoani
shinyanga, baada ya kukutwa katika mazingira yanayodaiwa kuwa ya kishirikina.
Watu hao waliojitambulisha kwa
majina ya Mwajuma Mponi (70) wa Nduku, na Shija Nkwabi(80) wa Nyashimbi wilayani
humo, wameanguka kijijini hapo wakitokea kijiji cha nduku wiyani humo wakielekea
Nyihogo Kahama kwa shughuli za kishirikina.
|
HAPA AKITEMA MAPOVU HUKU AKISEMA ANA NJAA SANA.
Katika maelezo yao wazee hao
wamedai kuwa wameanguka baada ya kutokea
ajali ya kishirikina huko angani, ambapo waligongana na wenzao ambao hawakuwafahamu
walikotoka na walikokuwa wanaelekea.
HAPA BIBI AKISAIDIWA KUINUKA BABADA YA KUVALISHWA NGUO NA WASALIMIA WEMA
Sambamba na hayo imeelezwa
kuwa wazee hao walikuwa uchi wakati wakianguka kabla ya kusaidiwa nguo na mama
mmoja wa maeneo ya Kafe Latino barabara ya Mhongolo.
Jeshi la Polisi la Wilayani humo likiri kutokeakwa
jambo jambo hilo na kwamba uchunguzi bado unaendelea na taarifa zitatolewa
baadaye.
0 comments:
Post a Comment