Imekuwa kama mazoea kwa Watanzania wengi pindi wanapomuona Kijana mwenzao amefanikiwa huwa wanaanzisha story tofauti. Hii imetokea kwa watu wengi sana hapa mjini na pengine kuchafua kabisa majina yao maana maneno hayo yamekuwa yakitawala akilini mwa watu siku hadi siku na kuwajengea imani kuwa ni kweli.
Robby ambae ni mfanyabiashara maarufu wa maduka ya nguo Jijini Dar es salaam amekuwa ni mmoja wa watu ambao wanasumbuliwa sana na tuhuma za kuwa ni member wa Freemason, katika kupata ukweli wa jambo hili leo nimeongea na Robby One kuhusu issue nzima ya watu kumuhisi yeye ni Freemason kutokana na maendeleo / mafanikio yake makubwa katika biashara yake.
Robby amefunguka na kusema kuwa si kweli kwamba yeye ana sali kwenye kanisa la Freemason wala hana uhusiano na Jumuiya hiyo, pia anashangazwa na watu wanaomzushia maneno kuwa yeye ni mwanachama. "Nashangaa vijana wananipigia simu mara nyingi na kuniomba niwapeleke kwenye Kanisa la Freemason ninalo sali" alisema na kuongezea "Naomba vijana wenzangu tuachane na hizi habari na kunipigia simu kuniomba niwapeleke kweye hilo kanisa maana sijui lilipo wala sina uhusiano nalo"
Moja kati ya ujumbe wa meseji aliotumiwa ni huu " Naomba kuuliza samahani lakini felmasn wako wapi? naomba nisaidie kama unawajua samahani lakini " ujumbe huo umetumwa kutoka namba 0*** ****42
Amewataka vijana wa Kitanzania wafanye kazi kwa bidii na kuachana na habari za uzushi ambazo zinawapotezea muda wao, Siri kubwa ya mafanikio yake ni kufanya kazi kwa bidii na sio kama wanavyodhani baadhi ya watu.
0 comments:
Post a Comment