VIDEO YA KALA PINA NA CHID BENZ WALIVYOZICHAPA.
Written By warrior on Tuesday, May 7, 2013 | Tuesday, May 07, 2013
CHEK VIDEO YENYEWE HAPA.....
PINA AZUNGUMZIA JUU YA TUKIO ZIMA...MSIKLIZE HAPA
"Ukweli ni mambo ya fedheha, mdogo wetu Chidi Benz, nnacho weza kusema mdogo wetu ni kwamba unga anaovuta sasa hivi unampeleka pabaya umeona eeh, tena mimi kama kaka yake namshauri aachane na matumizi ya madawa ya kulevya kwasababu mwisho wake utampeleka pabaya, mimi niko back stage nna show yangu nipo kazini, tupo seious watu wa hiphop, miaka mingi tulikuwa tuna nadi amani hatutaki matatizo na watu unaona bana, hawa ni watu ambao kwa namna moja ama nyingine wanasababisha hiphop ishindwe kwenda mbele na kusababisha hiphop ishindwe kwenda mbele na kuwapa mafanikio watu wa hiphop.tumeandaa show yetu nzuri, ilikua bonge ya show moja kali ya hiphop Tanzania kuwahi kutokea, show ambayo imekutanisha wasanii wakali wa hiphop ambao sasa hivi wanavuma, mi niko back stage naskia sauti ya Chidi Benz ameshika mic, muda ambao mi natakiwa kuwa stage naperfom, sa Chidi Benz ametokea wapi mbona kwenye ratiba yetu ya show hayupo, anaongea ubabe anakamba.yupo stage mi niko back stage bado, mi nikawaambia watu wangu vipi, huyu mtu mbona mnamuachia anatuharibia show? hasa watu ujue, ujue msanii, yaani jana ndio nimekubali msanii ni mtu mwenye hadhi na heshima kubwa sana sema Chidi Benzi amejishushia hadhi yake na heshima yake .Watu wakawa wanashindwa kumfanya kitu wakiangalia huyu ni mtu maarufu anajulikana, watu wakawa wanamplease kiustaarabu, Chidi eeh shuka hii show haikuhusu, sasa watu walivyokuwa wanamplease akawa anaona labda watu mafala au nini umeona eeh.
sasa mimi kitendo kimechukua kama dakika saba au nane hivi, bado yuko tu stage ameng'ang'ania, ananichelewesha mimi muda wa kuperfom, watu wanataka kuona show yangu, watu wamelipa hela zao, wameacha shughuli zao waje kumuona kalapina, ye anataka kuzkwaza watu wasimuone Kala pinia, huyu mtoto si adui jamani......." amesema Kala Pina ..endelea kumsikiliza hapo chini
Labels:
bongo
0 comments:
Post a Comment