Na Waandishi Wetu
MWANAHIP HOP Langa Kileo amezikwa Jumatatu iliyopita na mazishi yake yameacha maajabu kadhaa kwa baadhi ya waombolezaji kuanzia nyumbani kwao, Regency Estates, Mikocheni hadi alipokuwa akipelekwa Makaburi ya Kinondoni jijini Dar.

MAAJABU
Shughuli za kuuaga mwili wake zilifanyika nyumbani kwao, Regency Estates. Wakati wa kuuaga mwili wa marehemu ulipowadia, mmoja wa washikaji wa Langa ambaye hakufahamika jina lake, aliinama na kuushika mwili wake uliokuwa ndani ya jeneza kisha akaupiga busu.
Kama vile haitoshi, mshikaji huyo aliendelea kuonesha maajabu hayo huku watu mbalimbali wakilalamika kutokana na kitendo chake.

Ilibidi nguvu za ziada zitumike ndipo mshikaji huyo alipouachia mwili huo na kupisha waombolezaji wengine wapate fursa ya kuuaga.
Tukio lingine lililowashangaza waombolezaji msibani hapo ni kitendo cha Mchungaji wa Kanisa la Miito ya Baraka, Andulile Bwile kuifagilia Hip Hop ya Langa na kusema mashairi yake yalikuwa yakimkuna na kumpa ujumbe mzito tofauti na washika dini wengine ambao mara nyingi muziki huo huuponda na kuuita muziki wa kidunia.

MASELA WAKATAA INJILI, WATAKA HIP HOP
Wakati wa kuelekea makaburini ulipowadia, gari aina ya Fuso la Kanisa la Miito ya Baraka lilikuwa likipiga muziki wa Injili kwa ajili ya kuomboleza, lakini masela waligoma na kutaka nyimbo za marehemu Langa za Hip Hop ndiyo zipigwe badala ya zile za Injili.
“Hatuwezi kuvuta ‘feelings’ kwa nyimbo hizi, kwa nini nyimbo za msela wetu zisipigwe?” alihoji msela mmoja na kuungwa mkono na wenzake.
Hata hivyo, lengo la masela hao halikufanikiwa kwa kuwa lilipingwa kwa nguvu zote na kamati iliyokuwa ikisimamia mazishi hayo.

FAMILIA YAACHIA WATU WAJIACHIE
Familia ya marehemu Langa, haikuwa na cha kuficha juu ya kifo cha mtoto wao, haikumbagua yeyote kwani iliwaachia watu wa aina mbalimbali watoe nasaha na kueleza jinsi walivyomfahamu Langa.
Baada ya familia kutoa nafasi hiyo, vijana wa kitaa walianza kuelezea jinsi walivyoishi na marehemu. Vijana hao walipomaliza, Pili Misana ambaye ni mmiliki wa kituo cha kupambana na madawa ya kulevya, alimuelezea marehemu alivyofika kwenye kituo chake kilichopo Kigamboni jijini Dar na kuanza harakati za kuachana na matumizi ya madawa hayo.

MTOTO WA JK AWA PAPARAZI
Katika tukio lingine, mtoto wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, aitwaye Miraji aligeuka kuwa mpiga picha.
Miraji alichukua jukumu hilo mara baada ya mwili wa marehemu kufika katika makaburi ya Kinondoni.
Miraji pamoja na ndugu yake Ridhiwani, hivi karibuni wamekuwa wakijitolea kushiriki katika mazishi ya mastaa mbalimbali.
Awali walishiriki katika msiba wa Albert Mangweha ‘Ngwea’ na mume wa Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa, marehemu Jaffary Ally.
Mungu ailaze roho ya marehemu Langa Kileo mahali pema peponi

0 comments:
Post a Comment