Mwanasoka bora wa dunia Lionel Messi ametuhumiwa kukwepa kulipa kodi ya kiasi cha £3.4million.
Mashataka yamefunguliwa dhidi ya mshambuliaji huyo wa Barcelona na baba yake mwendesha mashtaka wa kaskazini mashariki mwa Catalunya, mahala ambapo Messi anaishi.
Wote wawili Messi na, Jorge Horacio, wanatuhumiwa kwa makosa matatu dhidi yao kwa kudanganya taarifa juu ya ulipaji kodi ambayo inafikia kiasi cha £3.4m cha kodi ya mapato katika miaka ya 2007, 2008 na 2009.
Jaji katika mahakama inabidi ayakubali mashtaka ya mwendesha mashtaka kabla ya kesi kufunguliwa rasmi.
0 comments:
Post a Comment